Harry Kane alifunga bao la kwanza dakika ya 13, kabla ya Erik Lamela 'Rabona' aliyesajiliwa kwa Pauni Milioni 30 kuongeza la pili dakika
ya 29 na la tatu kipindi cha pili.
Kane akakamilisha hat-trick yake kwa mabao mawili zaidi dakika za 75 na 81, kabla ya kipa wa Tottenham, Hugo Lloris kutolewa kwa kadi nyekundu.
Kane akaenda kusimama langoni kwa kuwa tayari timu hiyo ilikuwa imekwishakamilisha idadi ya wachezaji watatu wa kubadilisha. Mchezaji wa Asteras Tripolis aliyetokea
benchi, Jeronimo Barrales alifunga kwa mpira wa adhabu akimtungua Kane, ambaye jitihada zake za kuokoa hazikufanikiwa.
Chapisha Maoni