WAKATI nyota wa muziki wa Hip Hop, Rashid Makwiro ‘Chid Benz’ akikamatwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akiwa na madawa ya kulevya akiwa njiani kuelekea Mbeya,
Rehema Chalamila ‘Ray C’ aliyekuwa
amemfungulia kesi ya kumpiga katika kituo cha Polisi cha Oysterbay, amefuta shauri hilo nabkumsamehe.Akipiga stori na gazeti hili, Ray C alisema
ameamua kumsamehe kwa sababu yeye ni mtu wa Mungu na anaamini yanayomtokea ni ishara ya kumtambulisha kuwa matumizi ya dawa za kulevya hayafai.
“Mimi ni mtu wa Mungu, nimemsamehe na wala sitaki kesi naye, lakini kumsamehe mimi peke yangu hakusaidii, Watanzania wote kwa pamoja tumuombee ili jambo hili limalizike na likiisha, ninamuomba aje tushiriki pamoja katika tiba ya
Methadone,” alisema.
Ray C maarufu kama kiuno bila mfupa, alitoa kauli hiyo muda mfupi baada ya kuandika waraka katika akaunti yake kwenye mtandao wa Instagram,
akimsihi Chid Benz kuachana na matumizi hayo ya madawa ya kulevya.
Nyota wa muziki wa Hip Hop, Rashid Makwiro ‘Chid Benz’. “Pole kaka yangu Chid Benz, naumia kuona tatizo
ulilokuwa nalo bado haujalitafutia jibu, mimi ni dada yako na tumeshafanya kazi pamoja.
Tatizo ulilonalo na mimi nilishakuwa nalo na niliweza kulitatua sababu nilijitambua na kutafuta suluhu,
nimejaribu kila njia kukushauri badala yake ukaja na rungu la kimasai na kunitandika nalo nyumbani kwangu,” yalisomeka baadhi ya maandishi yake mtandaoni.
Ray C aliendelea kuandika kuwa kitendo cha kukamatwa kwake na madawa hayo kitakuwa ni jibu zuri kwake kuwa anakoenda si salama na kumtaka abadili njia na kuungana naye kwenye tiba ya Methadone kwani ndiyo kiboko ya madawa ya kulevya.
Kamanda Nzowa:
Chid Benz alikamatwa akiwa na kete 14 za madawa ya kulevya pamoja na misokoto miwili ya bangi hadi gazeti hili linakwenda mtamboni, alikuwa bado hajafikishwa mahakamani kukabiliana na tuhuma hizo.
Chapisha Maoni