TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) imeanza uchunguzi wa tuhuma za ufisadi wa Sh bilioni 40, uliotajwa kufanyika katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza.
Mkurugenzi wa TAKUKURU, Dk Edward Hoseah alisema jijini Mwanza jana kuwa tayari timu ya wachunguzi 148 wameshawasili jijini kuanza uchunguzi huo ambao umekwishaanza, ingawa
hakuweka bayana timu hiyo itakamilisha lini uchunguzi huo.
“Tayari Takukuru tumeshaleta timu ya mawakili wachunguzi 148 ambao wamepewa jukumu la kuchunguza na kuendesha suala la ufisadi wa
fedha katika jiji la Mwanza”, alisema.
Hivi karibuni Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa nchini (LAAC) ilifanya ziara yake jijini Mwanza ambapo ilibaini ubadhirifu wa Sh bilioni 40 na kutoa mapendekezo ya kufutwa kwa jiji hilo kutokana na ubadhirifu huo.
Chapisha Maoni