0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Stephen Wassira, amekitaka chama Cha Mapinduzi (CCM), kutokufanya makosa ya kusimamisha wagombea wasiokubalika katika
uchaguzi wa serikali za mitaa.

Wassira alisema mwaka 2010 CCM ilifanya makosa katika baadhi ya maeneo kwa kusimamisha wagombea wasiokubalika, hatua ambayo ilisababisha chama kupoteza majimbo na kata ambazo zilichukuliwa na upinzani.

“Naomba makosa ya mwaka 2010 yasijitokeze tena kwa kuwachagua watu wasiopendwa na wananchi, hali hiyo inaweza kusababisha nafasi
za wenyeviti wa setikali za mitaa na vitongoji zikaenda kwa wapinzani,’’ alisema.

Wassira alitoa tahadhari hiyo alipokuwa akifungua mkutano uliowashirikisha majumbe kutoka Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Mkoa wa Pwani.

Alisema mwaka 2010 makosa yalijitokeza kwa kupitisha majina ambayo wananchi hawakutaka
yarudi na kusema kuwa kosa hilo lisirudiwe mwaka huu bali wapitishe majina yanayokubalika. “Kama hamtayafanyia kazi majina hayo, mjue wapinzani watazichukua nafasi
hizo,” alitahadharisha.

“Tusiangalie mtu aliyeshinda kwa kupata alama nyingi, kinachotakiwa ni kuangalia huyo anakubalika kwa jamii na anavigezo vyoye kama hakubaliki inabidi asichukuliwe, mkifanya maamuzi
yasiyo sahihi, mtasababisha chama kukosa ushindi,’’ aliongeza.

Chapisha Maoni

 
Top