0
ARSENAL imelazimishwa sare ya kufungana mabao 3-3 na Anderlecht katika mchezo wa Kundi D Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku huu Uwanja wa Emirates, London.

Arsenal iliongoza kwa mabao 3-0 kabla ya kutepeta na kutema pointi mbili, kufuatia Aleksandar Mitrovic kuwafungia Wabelgiji bao la kusawazisha dakika ya mwisho ya muda wa kawaida.

Mkwaju wa penalti wa Mikel Arteta na mabao mengine ya Alexis Sanchez na Alex Oxlade- Chamberlain yaliifanya The Gunners iuanze vizuri mchezo.

Mchezaji wa zamani wa Portsmouth, Anthony Vanden Borre alianza kuisawazishia Anderlecht, ingawa alionekana ameotea kabla
ya kufunga tena Vanden Borre kwa penalti baada ya Nacho Monreal kufanyiwa madhambi.

Mchezo mwingine wa kundi hilo, Borussia Dortmund imeichpa 4 – 1 Galatasaray, mabao yake yakifungwa na Marco Reus dakika ya 39,
Sokratis Papastathopoulos dakika ya 54, Ciro Immobile dakika ya 73 na Semih Kaya aliyejifunga dakika ya 84, huku bao la wapinzani wao likifungwa na Hakan Balta dakika ya 69.

Dortmund sasa inatimiza pointi 12 kileleni mwa Kundi D, wakati Arsenal inafikisha pointi saba katika nafasi ya pili, baada ya timu zote kucheza mechi nne. Anderlecht ina pointi
mbili na Galatasaray pointi moja, japo nazo zimecheza mechi nne pia kila moja.

Kikosi cha Arsenal kilikuwa; Szczesny,
Chambers, Mertesacker, Monreal, Gibbs,
Arteta/Flamini dk62, Ramsey, Oxlade-
Chamberlain/Rosicky dk81, Sanchez, Cazorla,Welbeck/Podolski dk82.

Anderlecht: Proto, Vanden Borre, Mbemba/ Dendoncker dk54, Deschacht, Acheampong, Tielemans, Kljestan, Najar, Praet, Conte/ Kawaya dk45 na Cyriac/Mitrovic dk62.

Chapisha Maoni

 
Top