HUDUMA ya maombezi ya Good News for all Ministry imeandaa maombi maalumu kwa ajili ya kumuombea Rais Jakaya Kikwete ili afya yake iweze kuzidi kuimarika na kurejea nchini
kuendelea na majukumu yake ya kuwatumikia Watanzania.
Maombi hayo yatafanyika Mapinga, Bagamoyo, karibu na Shule ya Sekondari ya Baobab, mita chache katika barabara inayoelekea TAMCO.
Mwenyekiti wa Huduma hiyo, Askofu Charles Gadi alisema viongozi wa huduma hiyo, watafanya maombi hayo kuanzia leo hadi Rais Kikwete,
aliyefanyiwa upasuaji wa tezi dume mwishoni mwa wiki, atakaporejea nchini.
Gadi alisema Watanzania wanaalikwa kumuombea Rais Kikwete hususan siku za mwishoni mwa wiki, ambapo Jumamosi kutakuwa na maombi
maalumu ya kumtakia heri Rais.
“Kwa wengine wasioweza kuhudhuria maombi haya, wanatakiwa kushiriki nasi kwa kufunga na kuomba katika maeneo wanayoishi na kwa ajili ya kumuomba Rais ili afya yake iweze kuimarika,”
alisema Askofu Gadi.
Chapisha Maoni