0
Bi harusi wa miaka 14 nchini Nigeria ameshtakiwa kwa kuwaua watu wanne akiwemo mumewe wa miaka 35 baada ya kuweka sumu ya panya katika
chakula alichoandaa kwa sherehe za haruysi yake.

Kesi hiyo imewashangaza wahaharakati wa haki za kibinaadamu ambao wamesema kuwa msichana aliyeozwa kwa mume aliye mara mbili umri wake
anafaa kuchukuliwa kama mwathiriwa na wala sio muhalifu.

Wasila tasiu kutoka familia masikini katika eneo la waislamu la kazkazini huenda akakabiliwa na kifo
iwapo atahukumiwa.

Shahidi wa kwanza wa kiongozi wa mashtaka Lamido Abba Sorron-Dinka alikuwa msichana wa miaka 7 anayejulikana kama hamziyya,ambaye
alikuwa akiishi katika nyumba moja na Tasi'u pamoja na mumewe Umar sani,wakati bi haru huyo alipoweka sumu ya panya katika chakula
hicho.

Hamziyya alijulikana tu kama dadaake mke wa kwanza wa bwana Sani,mwanamke aliyeolewa na
marehemu awali katika eneo ambapo ndoa za wake wengi zimekithiri.

Msichana huyo wa miaka 7 alisema kwamba Tasi'u alimpa fedha ili kununua sumu ya panya kutoka duka moja jirani mnamo tarehe 5 mwezi Aprili,siku
ambayo bwana Sani alifariki.

''Alisema kuwa panya wanamsumbua katika chumba chake'',Hamziyya aliiambia mahakama.Upande wa mashtaka baadaye ulisema kuwa badala yake Tas'u aliweka sumu hiyo ya
panya katika chakula ambacho alikuwa amekiandaa kwa sherehe za baada ya harusi kwa kuwa alijuta uamuzi wake wa kumuoa bwana Sani.

Msichana huyo alikataa kuzungumza mahakamani. Jaji Mohammed Yahaya,katika mahakama ya
Gezawa alitoa hukumu kwamba Tasi'u ambaye alikataa kuongea katika mahakama hana hatia katika kusikizwa kwa kesi mnamo mwezi Octoba
ambapo alisomewa mashtaka.

Jaji huyo alikataa ombi la upande wa mshtakiwa la kesi hiyo kupelekwa katika mahakama ya watoto.

Ushahidi wa Hamziyya uliungwa mkono na Abuwa Yussuf muuzaji duka katika mji wa Unguwar Yansoro ambaye alithibitisha kuuza sumu hiyo
kwa mtoto huyo.

Jirani ya Bwana Sani mwenye umri wa miaka 30 ambaye ni mkulima, Abdulrahim Ibrahim alitoa ushahidi ambapo alisema kwamba alipewa chakula hicho kilichopikwa na Tasiu.''Nilipoletewa chakula
hicho niliona vipande vipande vyeusi''aliiambia mahakama.

Alikula vipande vinne vya madonge
vilivyotengezwa na maharagwe lakini hakupendelea ladha yake'',alisema na kuongezea kuwa ni Umar
pekee aliyeendelea kula.

Baadaye alisema kuwa alimuona bwana Sani katika bustani ,akiwa mgonjwa na kumpeleka nyumbani.

Lakini alipokuwa akijaribu kumuuguza bwana sani ,aligundua kwamba watu wengine watatu ambao walikuwa wamekula chakula hicho
wamefariki kwa ghafla.

Viongozi wa mashtaka walidai kwamba chakula cha Tasiu kilichowekwa sumu kiliwaua watu wanne na hivyobasi kuwajumuisha wanne hao katika kesi
moja ya mauaji.

Nigeria haijawahi kumyonga mtoto aliyefanya uhalifu tangu mwaka 1997,ambapo taifa hilo liliongozwa na dikteta Sani Abacha,kulingana na
shirika la kibinaadamu la Human Rights Watch.

Chapisha Maoni

 
Top