0
Mahakama Kuu ya Tanzania imemuachia huru aliyekuwa Katibu wa Taasisi za Kiislam, Sheikh Ponda Issa Ponda baada ya kuona hana hatia
dhidi ya Kesi ya madai ya Ardhi ya Agrekanza inayomilikiwa na Afidhi Self iliyokuwa inamkabili.

Akisoma Mashtaka hayo Mwanasheria wa Serikali, Tumaini Kweka mbele ya Jaji, Augustino Shangwe alisema baada ya kupitia vifungu vyote mahakama
imejiridhisha na kuona Sheikh Ponda hana hatia yoyote na kumuachia huru tangu leo lakini katika hali ya kushangaza Sheikh Ponda amerudishwa
rumande akisubiri kesi nyingine ya madai ya uchochezi, Mkoani Morogoro inayomkabili.

Chapisha Maoni

 
Top