MWENYEKITI ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Ilala Mhe. Mussa Azzan Zungu: Wananchi wanataka kujua ukweli, na anatoa nasaha zake ili bunge lisilete fujo
Tundu Lissu: Anaomba radhi ya kauli ya jana kuhusu tuhuma ya wakili kumuua mkewe.
Escrow: Muhongo kapotosha, viambatanisho haviwakilishi alivyosema. Muhongo ameleta vitu viwili tofauti na ni upotoshaji mtupu. Pesa za
Escrow ni za umma au binafsi, Muhongo anasema ni za makampuni na PAC inasema ni pesa za umma. Isingekuwa za umma amri ya kutolewa zisigetolewa kwa ushauri wa mwanasheria mkuu
wa serikali.
Benno Ndulu asingesema siwezi kutoa bila ridhaa ya waziri mkuu na raisi, pesa za binafsi iweje zitolewe kwa mlolongo wa mawaziri, Ili PAP wapate pesa ilikuwa lazima wapate ridhaa ya
Muhongo lakini hawajapa.
Nyaraka zinathibitisha mgao wa hizi fedha, zimepelekwa benki binafsi na ndani ya siku moja baadhi ya watendaji wa serikali wamelipwa.
Mgao wa fedha za Escrow kwa maafisa wa umma, maaskofu na wabunge ndani ya siku 1 (bilioni 78); ni pesa za umma.
Mpaka majaji wamehongwa milioni 400 eti michango ya harusi! Hizi fedha ni fedha za wananchi wa nchi hii! Kuna ushahidi wa kutosha katika ripoti ya PAC (TRA, CAG wamekiri)
Lazima watu wawajibike! Hizi ni fedha za Umma. Kumwondoa Rais ni vigumu kidogo. Tuanze na Waziri Mkuu, Muhongo, Tibaijuka, Werema na
majizi yote! Hawa tunawaweza.
Mahakama zetu katika hili hazina mamlaka ktk kesi hii ya IPTL.
Kwa ushahidi huu, ni ngumu kuwaamini majaji wetu na mahakama zetu.Kuna mawasiliano lukuki kati ya Ofisi za Umma katika utoaji wa fedha za
Escrow. Haziwezi kuwa fedha binafsi.
Fedha hazikutakiwa kutolewa na benki na haiwezi kufundishwa kazi na mwanasheria mkuu, Chombo pekee cha kutoa ushauri wa kodi ni TRA na sio
mwanasheria mkuu na katibu mkuu wa fedha hawezi kujificha nyuma ya kivuli cha ushauri wa mwanasheria mkuu.
Waliokuwa na mamlaka hawakufanya hivyo lazima wawajibike.
Waziri mkuu anatakiwa awajibike kwa sababu alikua anafahamu juu ya hili swali, na barua zote zilinakiliwa kwa waziri mkuu, ni kiongezi anaeshughulikia shughuli za kila siku za serikali.
Usalama wa taifa na financial inteligence unit chini ya wizara ya fedha hawakutimiza wajibu wao nao
hatuwezi kuwaacha.
Waziri wa nchi ofisi ya Raisi (Marry Nagu) amesimama kuelezea kutajwa raisi katika kashfa, anaomba watu wajadili kwa ustaarabu kufika
maamuzi pia kutotumia majina ya majaji.
Mwenyekiti amesimama na kusema anakubaliana nae pia anaomba watu wasitumie vijembe
Lissu: Anakana kutumia jina la raisi kwa dhihaka, na anarudia aliyoyasema. Wazuri kupewa hongo ni jambo baya, pia mwanasheria mkuu wa zamani kupewa hongo pia viongozi wa dini na
inafedhehesha taifa.
Hakimu kupewa milioni 400
na kampuni ambayo ilikua mahakamani 20. Jambo baya fedha za serikali kuibiwa. (Anataka kuongolea Mkono Adv lakini kengele inagonga na
kukaa chini)
Chapisha Maoni