Luteni kanali Yakouba Isaac Zida, ameteuliwa na rais wa mpito, Michel Kafando, kua Waziri Mkuu wa Burkina Faso, Novemba 19 mwaka 2014,
Ouagadougou.
Rais wa mpito wa Burkina Faso Michel Kafando amemteua luteni kanali Isaac Zida kuwa Waziri Mkuu. Awali luteni kanali Yacouba Isaac Zida amesema yuko tayari kushikilia wadhifa wa Waziri
mkuu iwapo atateuliwa. Luteni kanali Yacouba Isaac Zida anatazamiwa kwa
upande wake kuunda Baraza la mawaziri 25 Alhamisi Novemba 20 kukabiliana na changamoto ambazo rais wa mpito, Michel Kafando, amezibainisha siku ya
Jumanne Novemba 18 wakati wa kuapishwa kwake na ambaye anatumaini kuwa wananchi wa Burkina
Faso watachangia kikamilifu kutatua matatizo hayo.
" Nataka kuwaambia kwamba nimepokea majukumu haya kwa heshima kubwa, lakini pia kwa
unyenyekevu mkubwa", rais mpya wa mpito amesema katika hotuba yake ya kwanza aliyoitoa Jumanne Novemba 18.
Rais Michel Kafando ameongeza kwamba "unyenyekevu wa mtu
unaonekana pale anapoheshimu muda wa madaraka anaopewa kwa kipindi cha mpito, unyenyekevu wa mtu pia ni kufahamu kwamba cheo ni dhamana".
Sherehe za kuapishwa kwa rais huyo wa mpito zilifanyika katika mazingira mazuri, huku hotuba yake ikidumu dakika nne tu, akiwataka raia wake kuwa na heshima na maadili na kuwa pia na wajibu wavkwenda mbele.
Sherehe za kuapishwa kwa rais wa mpito Michel Kafando zilitamatisha utawala wa kijeshi uliyoongoza
nchi kwa kipindi cha siku 16 baada ya maandamano ya raia yaliyouwangusha utawala wa Blaise Compaoré aliyoongoza taifa hilo kwa kipindi cha
miaka 27.
Michel Kafando atakabidhiwa rasmi madaraka Ijumaa Novemba 21, na atashikilia madaraka hayo kwa
kipindi cha mwaka mmoja hadi utakapofanyika uchaguzi mkuu wa rais na wa wabunge mwezi Novemba mwaka 2015.
Chapisha Maoni