AMA kweli majanga yakimkuta binadamu hayapigi hodi! Daktari wa meno aliyejulikana kwa jina la
Dokta Ngariba (54), amejikuta ndani ya janga la tuhuma za ngono baada ya wapiga picha wa Oparesheni Fichua Maovu (OFM) kunasa sakata lake na mwanamke aliyedai ni mgonjwa wa jino
Tukio hilo la kushangaza lilijiri Juni 9, mwaka huu ndani ya Kituo cha Afya cha Halmashauri ya Wilaya ya Temeke kilichopo Kigamboni jijini Dar ambapo timbwili hilo lilitokea.
ILIKUWAJE? Ilikuwa wakati OFM wakizunguka katika Jiji la Dar es Salaam kama ada kusaka matukio ndipo walipopita nje ya kituo hicho walisikia sekeseke kutokea kwenye chumba ambacho baadaye kilibainika na cha kung’olea meno.
UCHUNGUZI, UFUATILIAJI Katika uchunguzi na ufuatiliaji wa OFM, mgonjwa huyo alisikika akidai
kwa polisi waliofika kutuliza sakata kuwa, alijihimu kwenye kituo hicho kwa lengo la kung’oa jino lakini katika hali ambayo hakuitarajia daktari huyo
alimtaka kimapenzi naye akajikuta akitumbukia.
....Akiandaa zana za kazi.
HEBU SIKIA HII “Mimi nimekuja kung’oa jino, linaniuma leo sijui siku ya ngapi? Lakini huyu daktari nimefika akanitaka kimapenzi. Nilidhani anatania, baadaye nikagundua kuwa amedhamiria,” alisema mwanamke huyo ambaye
alikutwa ameshavua dera.
UTETEZI WA DAKTARI
Hata hivyo, daktari huyo hakumwacha mgonjwa wake huyo atambe kiasi
hicho, alijibu mapigo kwa kusema kuwa,
alimpokea mwanamke huyo kama mgonjwa wa jino na kumwingiza kwenye chumba cha kung’olea meno lakini ghafla alimwona akianza kuvua nguo zake kisha kumvua na yeye shati na
baadaye kutaka kufungua zipu ya suruali.
.....Wakiwa chumba cha kung'olea jino
Akiendelea kuzungumza mbele ya Polisi wa Kituo cha Kigamboni waliofika kwenye sakata hilo ndani ya chumba cha matibabu ya meno, daktari huyo
alisema: “Mimi sikuwa na nia mbaya, nilijua ni mgonjwa anataka tiba ya kung’olewa jino. “Sasa nikiwa katika maandalizi ghafla nikamwona anavua
nguo na kisha akanivaa mimi na kuanza kunivua shati. Nashangaa sana anaposema nilimtaka kimapenzi, si kweli jamani.”
MASWALI MAGUMU
Baada ya maelezo ya Dokta
Ngariba, OFM ilikuwa na maswali yake lakini haikupewa nafasi ya kuyauliza kwa vile walidandia ishu.
.....Wakielekea kituo cha polisi Kigambono. Swali la kwanza; kama kweli Dokta Ngariba alivamiwa na kuvuliwa nguo na mgonjwa huyo,
alipiga kelele kuomba msaada kutoka kwa watumishi wenzake? Swali la pili; mpaka mgonjwa anajivua nguo zake kisha kumvua yeye shati na
baadaye kuelekea kwenye fraizi ya suruali, yeye alikuwa anawaza nini akizingatia ni mgonjwa wa meno? Uwazi lilizungumza na Mganga Mkuu wa
Wilaya ya Temeke, Sylvia Mamkwe kuhusu sakata hilo ambapo alisema:
“Taarifa hizo nazisikia kwako, niko safarini, nitafuatilia. Kama ni kweli hatua zinachukuliwa kwa waajiri wake ambapo najua kwa kosa kama hilo ni kupoteza kazi.”
Chapisha Maoni