Na Mathias canal, Mufindi
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM, Miraji Mtaturu amewapongeza madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi kutokana na kazi kubwa waliyoifanya kwa ajili ya kuimarisha ulinzi wa fedha za umma ambazo huliwa na baadhi ya viongozi wachache serikalini.
Hivi karibuni Baraza la madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi lilimtuhumu Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Wilaya hiyo, Paulo Ntinika, kwa tuhuma za ubadhilifu wa Sh Milioni 291, 713, 462 ambazo zimetumika vibaya kupitia sekta ya ujenzi.
Taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Peter Tweve hivi karibuni ilihusu kazi za ujenzi
zilizoongezwa na watendaji wa Halmashauri hiyo kinyume na maelekezo ya sheria ya manunuzi
namba 40(1) ya mwaka 2005.
Hata hivyo kwa mujibu wa taarifa ya ukaguzi ya Julai Septemba 2014/2015, baadhi ya barabara zinazohusishwa na malipo ya nyongeza ni pamoja na
ya Kibengu hadi Kipanga yenye urefu wa km 37, barabara ya Kipanga B hadi Uhafiwa na barabara ya Mkuta Ludilo hadi Ilasa yenye km 21.
Taarifa hiyo ya ukaguzi inaonesha barabara ya Kibengu Kipanga, Januari 1, 2014 katika kikao cha zabuni kilitoa kazi kwa nyongeza yenye thamani ya
Sh 21,876,500 kwa ajili ya matengezo yake na kufanya thamani ya kazi yote kuwa Sh 313,956,500.
Mtaturu alisema kuwa tuhuma za msimamizi mkuu wa Halmashauri kushindwa kusimamia vyema fedha
za umma ni dhahiri kwamba kunaitajika ufafanuzi wa kina kutoka kwa kiongozi huyo kutokana na upotevu
wa fedha za umma.
"Kwa mujibu wa kanuni za uendeshaji wa Halmashauri Tanzania, madiwani wana wajibu wa kufanya kazi nzuri katika Halmashauri ili kuleta matokeo mazuri kwa wananchi waliowaamini na
kuwapa dhamana ya kuwachagua kuwa viongozi katika Kata zao" Alisema Mtaturu
Alisema kuwa kazi iliyofanywa madiwani hao ni wajibu wao wa kisheria huku akiwapongeza pia kwa kuunda tume itakayokuwa na wajumbe watano ili
kufanya uchunguzi wa sakata hilo.
Mtaturu alitoa wito kwa serikali kuchukua hatua za haraka kwa wale wote waliohusika na tukio hilo,
huku akieleza kuwa jambo hilo limeichafua Halmashauri hiyo hivyo ili kukuza heshima ya Halmashauri na watendaji wengine kuwa waoga
kufuja mali za umma ni lazima watakaobainika kuchukuliwa hatua kali za kinidhamu kulingana na
kanuni za utumishi.
Akizungumzia maandalizi ya uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika Disemba 14, mtaturu alisema
kuwa CCM imejipanga vyema nchi nzima ili kuongoza vitongoji na vijiji vyote Tanzania.
Chapisha Maoni