0
Jeshi la Nigeria linasema kuwa limelikomboa eneo la Chibok siku mbili baada ya wapiganaji Waislamu, Boko Haram, kushambulia mji huo.

Wasichana wa shule zaidi ya 200 walitekwa kutoka Chibok mwezi wa Aprili. Msemaji wa jeshi, General Olajide Laleye, alieleza kuwa mji umekombolewa lakini alikiri kuwa
operesheni bado haikukamilika na inaendelea.

Haikuelezwa hasara iliyopatikana.
Wapiganaji waliposhambulia Chibok siku ya Alkhamisi, wakaazi waliwashutumu wanajeshi kuwa walikimbia bila ya kupigana.


chanzo: BBC

Chapisha Maoni

 
Top