0
Aliyekuwa Rais wa Ivory Coast, Laurent Gbagbo, anayezuiliwa katika mahakama ya kimataifa ya ICC, ameteuliwa kama mgombea mkuu wa Urais wa chama cha kisiasa alichokuwa anaongoza,
kabla ya kuzuiliwa katika mahakama ya ICC.


Taarifa hii ni kwa mujibu wa chama hicho FPI ambacho Gbagbo alikianzisha.
Yote haya ni katika maandalizi ya uchaguzi mkuu utakaofanyika mwaka ujao.

Kamati ya chama hicho, imesema ni halali kwa Gbabgo kuteuliwa kugombea urais na hata kuongoza chama hicho alichokianzisha bwana Gbagbo.

Hata hivyo kuna mgombea mwingine ambaye tayari ameidhinishwa na chama hicho Affi N'Guessan ambaye pia amesisitiza uteuzi wa Gbagbo uondolewe hasa kwa kuwa anazuiliwa ICC.

Chama hicho kinajiandaa kufanya kongamano lake kuu Disemba kati ya tarehe 12-14. Gbagbo, mwenye umri wa miaka 69, anakabiliwa na tuhuma za uhalifu dhidi ya binadamu, akidaiwa
kuutenda wakati alipokataa kukubali matokeo ya uchaguzi ambapo alishindwa Novemba mwaka
2010.

Wafuasi wake, walikabiliana kwa miezi mitano, na wafuasi wa Rais Alassane Ouattara, aliyetangazwa mshindi wa uchaguzi huo. Watu 3,000 walipoteza
maisha yao.

Gbagbo alikamatwa mwezi Aprili mwaka 2011 na kikosi cha Rais Ouattara kikiungwa mkono na Ufaransa France na Umoja wa Mataifa.

Alipelekwa Hague Novemba mwaka uliofuata na kuwa rais rais wa kwanza wa zamani kufikishwa mahakamani ICC.
Gbagbo anatarajiwa kufikishwa kizimbani tarehe 7 mwezi Julai mwaka ujao. Uchaguzi wa Ivory Coast
umepangwa kufanyika Oktoba 2015.

Chapisha Maoni

 
Top