0
Kundi la wafanyakazi wa afya nchini Mali leo
wanapewa chanjo ya majaribio dhidi ya ugonjwa wa Ebola.

Hii ina maana kwamba watu waliojitolea kufanyiwa chanjo ya majaribio nchini Mali kufikia watu 40. Utafiti ulianza Mali kufuatia majaribio salama kufanyika nchini Uingereza na Marekani.

Chanjo hiyo imetengenezwa na wanasayansi katika Taasisi ya Taifa ya Mzio na Magonjwa ya Kuambukiza huko Maryland, nchini Marekani na
inatengenezwa na kampuni ya dawa ya Uingereza ya GlaxoSmithKline.

Kutokana na kupamba moto kwa maambukizi ya Ebola, Afrika Magharibi, kasi ya kupata chanjo inaendelea.

Chapisha Maoni

 
Top