0

Waziri wa Fedha na Mipango nchini, Dkt. Philip
Mpango, amefafanua adhabu ya kosa la kutotoa
ama kudai risiti katika manunuzi na kusema kuwa
serikali imefuta kipengele cha kufungwa na pia
faini itatozwa kulingana na ghamara ya bidhaa
itakayonunuliwa.
Akizungumza leo Mjini Dodoma na kupitia Shirika
la Habari la Taifa, Dkt. Mpango amesema kuwa
wameamua kufanyia marekebisho sheria hiyo
kutokana na maoni ya wadau mbalimbali lakini
bado adhabu itatolewa kwa mtu yeyote asietoa
ama kudai risiti wakati wa mauzo.
Dkt. Mpango amesema kuwa moja kati ya faida
kwa wafanyabishara katika kutoa risiti ni pamoja
na kuweka rekodi nzuri katika biashara lakini pia
na mnunuzi kujua ni kiasi gani umekatwa kwa
ajili ya kodi.
Amesema kuwa sheria waliyoiweka sasa adhabu
itatolewa kutokana na ukubwa wa mauzo ya
mfanyabiashara ili kuwalinda wafanyabiashara
wadogo ambao watakuwa wanatenda makosa
hayo ili kuwakumbusha umuhimu wa kutoa risiti
katika mauzo yao.
Ameeleza kuwa lengo kuu la kufanya hivyo ni
kujenga taifa lenye utamaduni wa kulipa kodi
lakini pia fedha hizo zitasaidia miradi mbalimbali
ya maendeleo ikiwemo katika sekta ya Afya, Elimu
na maeneo mengine.
Dkt. Mpango amesema kuwa wapo
wafanyabiashara wengine wanauza mamilioni ya
shilingi lakini hawatoi risiti za mauzo yao jambo
ambalo linaikosesha serikali mapato halali na pia
mnunuaji anakua hajui ni kiasi gani cha kodi
amekatwa kutoka na manunuzi ya bidhaa hizo.


Chapisha Maoni

 
Top