Waziri mkuu wa Uingereza, David Cameron,
ametangaza atajiuzulu, baada ya kushindwa
kuwashawishi raia wengi wa Uingereza, kusalia
katika Muungano wa Ulaya (EU).
Cameron akiwa amejawa na huzuni amesema
kuwa atasalia ofisini kwa siku tisini zijayo ndipo
ang’atuke.
Waziri Mkuu huyo aliyeongoza kampeni ya
kusalia katika muungano wa EU amesema kauli
hiyo imempa mshutuko mkubwa na kwa baadhi
ya watu mashuhuri duniani.
Akiongea katika kikao cha waandishi wa habari
nje ya afisi yake jijini London, Cameron amesema
kuwa hahisi tena kuwa mtu muhimu wa
kuliongoza taifa hilo kwa ufanisi chini ya uamuzi
kama uliofanywa.
Sauti yake iliibua hisia hasa aliposema "nalipenda
sana taifa hili na najihisi vizuri kuliongoza muda
huo wote."
Cameron amesema kuwa kauli ya wengi sharti
isikizwe japo hafahamu kwanini Waingereza
walichukua uamuzi kama huo ilhali taifa hilo
lilikuwa linaufanisi mkubwa sana ndani ya EU.
Cameron akiwa ameandamana na mkewe
amesema bila shaka sasa utawala mpya
unahitajika utakaoweza kutathmini mbinu na
mkataba wa kujiondoa kutoka kwa muungano
huo wa bara la Ulaya.
Nyumbani
»
HABARI
» Waziri Mkuu, David Cameron
atangaza kujiuzulu baada ya
Uingereza kupiga kura ya
kujitoa rasmi kwenye Umoja
wa Ulaya(EU).
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Chapisha Maoni