Mwenyekiti wa TLP taifa Dkt. Augustine Lyatonga
Mrema amesema kwamba kitendo cha Rais Dkt.
John Magufuli kusema kwamba siasa ziachwe
hadi miaka mitano iishe kunatokana na tabia ya
upinzani kugomea kila kitu bila kuweka maslahi
ya taifa mbele.
Dkt. Mrema ameyasema hayo leo alipokuwa
akizungumzia kuhusu kauli hiyo ya Rais na
kama haitaviathiri vyama kikiwemo chama
anachokiongoza cha TLP.
''Kwa maoni yangu binafsi hii imetokana na tabia
yetu sisi wapinzani kugomea kila kitu hata
mambo ambayo yana maslahi kwa taifa, kwa
mfano ukiangalia wakati Rais Dkt. John Magufuli
anazindua bunge la bajeti wapinzani walimgomea
na kutoka nje, hapa walianza kumhukumu kabla
hajaanza kazi''- Amesema Mrema.
Mrema ameongeza kuwa hata bunge la bajeti
linaloendelea wabunge wa upinzani wametoka
vikao karibu vyote wakati bajeti inayojadiliwa siyo
ya Naibu Spika ni bajeti ya serikali na kwamba
wangetumia kanuni za bunge kuweza kumuondoa
kama hawamtaki kuliko kuacha kuwakilisha
wananchi wao.
Aidha Mrema ameenda mbali na kusema kuwa
nchi hii haiwezekani kila siku ikawa ni
maandamano kwani wananchi wanatakiwa
wafanye kazi na kama wapinzani walikuwa na nia
ya dhati wangebakia bungeni wajadili kwanza
bajeti.
Kuhusu chama chake pia kutofanya siasa Mrema
amesema yeye hana maandamano ya kila mara
hivyo anaamini atakuwa na mikutano halali muda
ukifika lakini kwa sasa wananchi wafanye kazi
kwanza.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Chapisha Maoni