Mgawanyiko umeripotiwa ndani ya jeshi la Burkina Faso kuhusu ni nani anayefaa kuliongoza taifa hilo kufuatia kujiuzulu kwa rais Blaise Campaore baada
ya miaka 27 uongozini.
Kituo kimoja cha radio kilitangaza taarifa kutoka kwa naibu mkuu wa kikosi cha kumlinda rais kanali Isaac Zida iliyosema kuwa amechukua jukumu la
kuliongoza taifa hilo.
Mapema mkuu wa majeshi Honore Traore alitangaza kuwa alikuwa amechukua usukani Jen.Honore Traore
Blaise Compaore alijiuzulu baada ya kushuhudia maandamano yenye ghasia baada ya jitihada zake za kutaka kuliongoza taifa hilo kwa awamu
nyengine kupitia bunge kugonga mwamba.
Akizungumza hapo jana kanali Zida amesema kuwa Jenerali Traore hawezi kuliongoza taifa hilo.
''Nimechukua jukumu la kuliongoza taifa hili na serikali ya mpito ili kuliendeleza na kuhakikisha kuwa kuna mabadiliko ya kidemokrasia kwa njia ya amani'' alisema kanali Zida katika hotuba yake
katika runinga.
Chapisha Maoni