0
JAHAZI linazidi kwenda mrama! Wakati
shauri lao la kugawana mali likidaiwa
kufikishwa mahakamani, picha mpya
imenaswa ikionesha dhahiri kwamba
Mtangazaji Gardner Gabriel Fikirini Habash
‘Kapteni’ ameamua kusonga mbele na
maisha yake na kusahau kabisa kama
alikuwa na mke aitwaye Judith Daines
Wambura Mbibo ‘Jide’, Amani linakupa
mchapo kamili.
PICHA IPOJE?
Picha hiyo ambayo inamuashia ‘endiketa’ Jide kuashiria kwamba, Gardner amejiweka pembeni na kuwa bize na ‘starehe’ zake, inamuonesha mtangazaji huyo akiwa ‘ziro distensi’ na kabinti
kabichiii (jina halikupatikana mara moja)
katika bwawa la kuogelea (swimming
pol) huku wakiwa wamening’iniza miguu
kwenye maji.

PICHA ILIVYOVUJA
Kwa mujibu wa chanzo makini, picha
hiyo iliibwa katika simu ya binti huyo
aliyekuwa na Gardner kisha kuisambaza
katika mitandao ya kijamii bila yeye
mwenyewe kujua.

“Yule dada aliyekuwa na Gardner
aliibiwa picha hiyo na shosti yake katika
simu yake ndipo akaisambaza
mitandaoni,” kilisema chanzo hicho.

NI WAPI?
Mara baada ya mapaparazi wetu kunasa
picha hizo, kabla ya kumtafuta Gardner
ili kujua ukweli, walianza kusaka eneo
ambalo wawili hao walikuwa wakiponda
raha zao ambapo jitihada hizo zilikosa
majibu ya moja kwa moja.
“Hii ilikuwa ni Mikocheni, Escape One
siku hiyo kaka mkubwa alikuwa akifanya
yake si unajua tena ameshaona liwalo na liwe,” kilisema chanzo cha kwanza.

ETI NI KIGAMBONI
Chanzo kingine kilichozungumza na
mapaparazi wetu kilipishana na
mwenzake kwa kudai kuwa wawili hao
walikuwa katika ufukwe wa Southern
Sun Kigamboni wakijiachia kwa raha zao.
“Mimi kuna kuna mtu kanihakikishia
kabisa hii ilikuwa ni Kigamboni,
walikuwa wakiponda raha tena Gardner
siku hiyo inaonekana alikuwa ameonja
kidogo si unajua tena kaka mkubwa na
mambo yetu yale, Jide hana chake tena
pale,” kilinyetisha chanzo kingine.
Gardner akiwa na Lady Jaydee.

NDIYO ZAKE?
Wakati mapaparazi wetu wakiendelea
kuchimba data kuhusiana na mtangazaji
huyo ambaye alijizolea umaarufu
mkubwa katika Kipindi cha Jahazi cha
Redio Clouds FM, chanzo kingine
kilipenyeza madai kuwa, Gardner kwa
sasa ndiyo zake kujiachia na ‘totoz’
tofauti.

“Aaah…kwani nyinyi hamjui? Jiongezeni
bwana, Gardner kwa sasa ameshaondoa
mawazo kabisa kwa Jide na badala yake
anajipoza tu kwa totoz,” kilisema chanzo.

MAKABRASHA YA LIBRARY
Katika makabrasha yaliyopo katika
kumbukumbu za Magazeti Pendwa,
Gardner aliwahi kunaswa na kabinti
kengine katika Fukwe za Coco jijini Dar
wakiwa wamegandana kama
kumbikumbi.

GARDNER ASAKWA
Mapaparazi wetu juzikati walimfuata
Gardner katika Ofisi za EFM zilizopo
Mikocheni jijini Dar ambako mtangazaji
huyo anafanya kazi kwa sasa, mtu wa
mapokezi alidai hajafika.

ATUMIWA UJUMBE
Jitihada za kumpata kwenye simu
zilipogonga mwamba, mapaparazi wetu
walimtumia ujumbe mfupi wa maandishi
(SMS) kumsomea mashitaka yake na
kama ni kweli ameamua kumpotezea
mazima Jide.
Gardner hakujibu mapema, baadaye
alipigiwa simu, akapokea na kuambiwa
ajibu mashitaka yake kama alivyotumiwa katika SMS. Alijibu kuwa yeye ana marafiki wengi hivyo si kila
atakayeonekana naye basi ni mpenzi
wake. Msikie:

“Hivi kila mdada nitakayeonekana naye
atakuwa ni wifi jamani? Mi nina marafiki
wa jinsi zote, sina la kusema.”

UKWELI NI NINI?
Mapaparazi wetu walizidi kumtafuta
Gardner kujua ukweli wa picha hiyo na
eneo walilopigia lakini hakupokea tena
hivyo ukweli anaujua mwenyewe.

TUJIKUMBUSHE
Gardner na Jide waliofunga ndoa Mei 14,
2005 na kutobarikiwa kupata mtoto,
Agosti mwaka huu walidaiwa
kumwagana.

Chapisha Maoni

 
Top