0
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na
Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe
Liberata Mulamula aliyekwenda kumjulia
hali katika hospitali ya John Hopkins
iliyopo Baltimore, Maryland, nchini
Marekani, leo Jumapili, siku moja baada ya
kufanyiwa upasuaji wa Tezi Dume.
Habari kutoka hospitalini hapo ambazo
Globu ya Jamii imepata zinasema Rais
Kikwete anaendelea vyema na leo asubuhi alianza mazoezi ya kutembea, kuashiria kwamba mambo yote ni mswano.
Tutaendelea kuwashirikisha kwa taarifa
sahihi za maendeleo yake mara kwa mara.
Tuzidi kumuombea apate nafuu haraka ili arejee nyumbani kulijenga Taifa.

Chapisha Maoni

 
Top