KIPA Joe Hart amepewa mapumziko katika timu ya soka ya taifa ya England na hatakuwepo kwenye mchezo dhidi ya Scotland Jumanne- akimpa nafasi Fraser Forster kuichezea nchi
yake katika Uwanja wa klabu yake ya zamani, Celtic Park.
Kocha wa Three Lions, Roy Hodgson amesema amemuacha Hart nje ya kikosi cha kucheza mechi hiyo ya Glasgow baada ya kipa huyo namba moja wa Manchester City kuisaidia
England kuifunga Slovenia 3-1 Jumamosi.
Hodgson amesema: "Ninamruhusu Leighton Baines kwenye mchezo na Scotland, lakini pia ni majeruhi,".
"Mwingine ni Joe Hart. Atakwenda nyumbani kupumzika kwa sababu nina makipa wengine wawili naweza kuwachezesha.
Forster aliwahi kuichezea Celtic kabla ya
kuhamia Southampton na kipa mwingine kwenye kikosi cha Hodgson ni Ben Foster wa West Brom.
Chapisha Maoni