UGIRIKI imemteua Kostas Tsanas kuwa kocha wa muda wa timu ya taifa leo, ingawa hadi sasa hakuna uthibitisho wa kufukuzwa kwa Mtaliano Claudio Ranieri.
Shirikisho la Soka nchini humo (EPO)
limemsimamisha Ranieri huku panda zote mbili zikifanyia kazi mustakabali wa Mkataba baina yako wenye thamani ya Euro Milioni 1.6.
Ranieri, mwenye umri wa miaka 63, alitarajiwa kubaki Ugiriki hadi baada ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Serbia mjini Crete Jumanne, lakini mpango huo haupo tena.
"Shirikisho la Soka limetangaza kuteua
makocha wa muda watakaoiongioza timu kwenye mechi ya kirafiki na Serbia ambao ni Kostas Tsanas na Nektarios Pantazis," imesema taarifa ya EPO.
Mkuu wa EPO, Giorgos Sarris ameweka wazi juu ya mango wa bodi hiyo kuachana na Ranieri Jumamosi kufuatia kipigo cha 1-0 dhidi ya Faroe Islands ambayo inaiacha Ugiriki mkiani mwa Kundi F katika kampeni za kufuzu Euro
2016.
Ranieri aliteuliwa mwaka 2014 World Cup, akirithi mikoba ya Mreno Fernando Santos kwa mkataba wa miaka miwili.
Chini ya kocha huyo wa zamani wa Chelsea, Juventus na Monaco, Ugiriki imeporomoka mho
kiwango.
Chapisha Maoni