Makatibu wakuu wa CCM, Abulrahman Kinana na Dk Willibrod Slaa wa Chadema kesho watashiriki katika mjadala wa rais wa Tanzania anayetakiwa kupitia Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.
Mjadala huo utakaofanyika Dar es Salaam, umeandaliwa na Asasi ya Twaweza ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa ripoti ya utafiti wa maoni ya wananchi juu ya mwelekeo wa rais
wanayemtaka kupitia uchaguzi wa mwaka 2015.
Meneja Mawasiliano wa Twaweza, Risha Chande alisema viongozi hao wamethibitisha kushiriki.
Akitoa mwelekeo wa ripoti hiyo, Chande alisema imekusanya maoni mbalimbali ikiwamo uwezo na sifa za rais anayehitajika 2015, uwezo wa chama
chake, ahadi za wabunge 2010 na uamuzi wao 2015.
Wengine watakaoshiriki mjadala huo ni Naibu Katibu Mkuu wa CUF (Tanzania Bara) Magdalena Sakaya na Mhadhiri katika Idara ya Sayansi ya Siasa, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Benson
Bana. “Mjadala huo utatoa nafasi ya kuchambua kiongozi gani anayetufaa. Wachangiaji wote watapata nafasi ya kutoa ufafanuzi na tathmini zao, hivyo ni fursa kwa Watanzania wote kushiriki
kikamilifu katika mjadala huo,” alisema.
Chande alisema katika utafiti huo unaozinduliwa kesho, wananchi waliulizwa ni hatua gani wangependa kuona katika vyama vya kisiasa na
uongozi wake.
Utafiti huo uliopewa jina la ‘Sauti za Wananchi: Tanzania kuelekea 2015 Wananchi watoa maoni yao na matakwa yao juu ya uongozi wa kisiasa
nchini’, umefanywa na mtafiti wa Twaweza, Elvis Mushi.
Chande alisema mwendesha mada atakuwa Mkurugenzi mstaafu wa Twaweza, Rakesh Rajani.
-----------------------------------
Muda: 11:00am – 1:00pm (Saa tano asubuhi hadi saaa saba mchana)
Tarehe: Jumatano Novemba 12 2014
mahali: Makumbusho, (imetazamana na IFM)
-----------------------------------
Chapisha Maoni