0
Mahakama ya Mwanzo ya Riagoro wilayani Rorya mkoani Mara, imeteketezwa kwa moto na watu
wasiojulikana huku nyaraka muhimu zilizokuwamo ndani yake zikiteketea zote.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi Tarime/ Rorya, Lazaro Mambosasa, alisema wanalifanyia uchunguzi tukio hilo na inaonyesha haikutokana
na hitilafu ya umeme kutokana na kutokuwa na nishati hiyo.

Kamanda Mambosasa alisema moto huo uliteketeza chumba cha ofisi ya makarani kunakohifadhiwa nyaraka za mahakama vikiwamo vielelezo, lakini chumba cha hakimu kilinusurika
baada ya wananchi kufika eneo la tukio hilo na kusaidia kuzima moto.

Alisema kwa sasa Jeshi la Polisi linawasaka waliofanya tukio hilo ili wafikishwe mbele ya vyombo vya sheria.
Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya Tarime, Adrian Kilimi, alipotafutwa kwa simu kuelezea tukio hilo hakupatikana.

Chapisha Maoni

 
Top