0
Waziri wa Mashauri ya Nchi za Nje wa Urusi,
Sergei Lavrov, ameyashutumu mataifa ya magharibi kwamba yanataka kubadilisha serikali ya Urusi kwa kuiwekea nchi hiyo vikwazo vya
kiuchumi, kwa sababu ya mzozo wa Ukraine.

Aliuambia mkutano wa wataalamu wa mashauri ya nchi za nje mjini Moscow kwamba mataifa ya magharibi siyo yanataka kuifanya Urusi ibadilishe
sera zake kuhusu Ukraine tu, bali yanataka kubadilisha serikali ya Urusi.

Marekani na Umoja wa Ulaya zimeiwekea Urusi vikwazo kadha vya kiuchumi kwa sababu zinaishutumu kuwa inawasaidia wapiganaji wa
mashariki mwa Ukraine.

Bwana Lavrov alisema vikwazo hivyo vililenga kuharibu uchumi wa Urusi na kuchochea maandamano.

Chapisha Maoni

 
Top