Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imeyatupilia mbali maombi ya Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda
Issa Ponda ya kuitaka isimamishe kesi ya uchochezi inayomkabili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro hadi itakapotoa uamuzi wa rufaa yake.
Jaji Lawrence Kaduri aliyatupilia mbali maombi hayo baada ya kukubaliana na pingamizi la awali lililowasilishwa mahakamani hapo na upande wa
mashtaka.
Katika pingamizi hilo, Wakili Mkuu wa Serikali, Benard Kongola alidai kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kuzuia shauri hilo lisiendelee
kusikilizwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro.
Jaji Kaduri alikubaliana na pingamizi la awali la upande wa mashtaka na kuyatupilia mbali maombi yaliyowasilishwa mahakamani hapo na Sheikh Ponda kupitia wakili wake Juma Nassoro.
Wakili Nassoro aliiomba Mahakama hiyo itumie busara kusimamisha kesi hiyo kwa kuwa upande wa Jamhuri hautaathirika kwa kuwa ndiyo
uliofungua kesi hiyo.
Katika rufaa hiyo, Ponda anadai hakukuwa na ushahidi wa kutosha kumtia hatiani kwa mashtaka
yaliyokuwa yakimkabili. Ponda na wenzake walikuwa wakikabiliwa na
mashtaka ya kula njama, wizi wa mali yenye thamani ya Sh59.6 milioni kwa nia ya kujimilikisha ardhi inayomilikiwa na Kampuni ya Agritanza.
Chapisha Maoni