Kamati ya Maandalizi ya Mkutano wa Nne wa Dunia wa Maspika wa Mabunge, jana jumatatu, imeanza mkutano wake wa pili na wa siku mbili unaofanyika hapa Umoja wa Mataifa.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Anne Makinda ( Mb) ni miongoni mwa washiriki wa Kamati hiyo ya
Maandalizi ukiwahusisha maspika kadhaa kutoka mabunge mbalimbali duniani.
Katika mkutano huo wa siku mbili ambao umeandaliwa na Inter-Parliamentary Union ( IPU), wajumbe wa kamati hiyo wanajadili mapendekezo ya Maudhui na Tamko la Mkutano wa Nne wa Dunia wa Maspika wa Mabunge unaotarajiwa kufanyika mwaka 2015.
Aidha wajumbe hao wanatarajiwa pia
katika siku mbili hizi kutoa uamuzi wapi
kutakakofanyikia mkutano huo.
Maudhui na Tamko la mkutano huo wa Nne pamoja na mambo mengine yanatarajiwa kuwa yatazingatia vipaumbele au mambo muhimu na ya msingi ya mahitajo ya mwanadamu katika dunia ya sasa.
Mambo ambayo pia ni ajenda muhimu
katika Umoja wa Mataifa Baadhi ya mambo hayo na ambayo wajumbe wa kamati ya Maandalizi wanayapitia ni pamoja na, tathimini ya utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo ya Millenia ( MDGs), Mapokeo ya Agenda Mpya za Maendeleo Endelevu baada
ya 2015, na maadhimisho ya miaka 70 ya kuanzishwa wa Umoja wa Mataifa.
Katika siku ya kwanza ya mkutano wao
wajumbe wamesikiliza thathmini ya
utekelezaji wa MDGs, tathmini iliyotolewa
na Spika wa Bunge la Iceland ambaye
ameainisha mafanikio na changamoto
katika utekelezaji wa malengo hayo ambayo
yanafikia ukingoni mwakani.
Pamoja na kusikiliza tathimini ya MDGs,
Maspika hao pia wamepata fursa ya
kubadilishana mawazo na Mwakilishi
Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja
anayehusika na SDGs,
Bi Amina Mohammed ambaye ametoa
muhtasari wa ajenda na malengo mapya ya SDGs baada ya 2015. Katika maelezo yake Bi Amina ametilia mkazo ushirikiano kati ya Umoja wa Mataifa, Serikali na nafasi ya Mabunge katika utekelezaji wa SDGs huku
akisisitiza kwamba changamoto kubwa na muhimu katika utekelezaji wa SDGs hizo ni suala na uwezeshaji wa raslimali fedha, suala ambalo amesema linahitaji
ushirikiano wa pamoja katika kulipatia
muelekeo wake.
Aidha amewaeleza wajumbe wa Kamati
kuwa Maspika na wabunge katika kila
Bunge duniani kote wanapashwa kuwa
weledi na wenye ufahamu mkubwa kuhusu SDGs yenye ajenda 17 na malengo 169 kwa kuwa wao ndio wawakilishi halisi wa wananchi waliowachagua.
Akasisitiza kuwa wabunge wanapashwa
kushirikiana kikamilifu na serikali katika
utekelezaji wa SDGs na huku au kubemba ujumbe wa mambo muhimu na ya msingi kwa mahitajimasuala ambayo ni muhimu kwa maisha yana Maspika kadhaa ambao
ni wajumbe wa Kamati ya maandalizi ya
Mkutano wa Nne wa Dunia wa Maspika wa Mabungo utaofanyika mwakani.
Chapisha Maoni