Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Jaji Mkuu waTanzania Mhe Mohamed Chande Othman pamoja na ujumbe wake walipomtembelea na kumjulia hali
Jumapili Novemba 16, 2014 katika hoteli
maalumu jirani na Hospitali ya Johns
Hopkins jijini Baltimore, Maryland,
Marekani anakoishi baada kutoka katika
hospitali hiyo alikofanyiwa upasuaji wa
tezi dume.
Jaji Mkuu na ujumbe wake wako Marekani kwa ziara ya kikazi ambapo pamoja na mambo mengine yeye na ujumbe wake watahudhuria mkutano maalumu wa kimataifa wa Mabadiliko ya Sheria ya Ushahidi jijini Washington na pia kukutana na taasisi mbalimbali za fedha na marafiki wa maendeleo katika ili kupata wabia wa ujenzi wa maendeleo ya mahakama.
Wengine kutoka kushoto ni Balozi wa
Tanzania nchini Marekani Mhe Liberata
Mulamula, Jaji wa Mahakama ya rufani
Mhe Ibrahim Juma, Msajili wa Mahakama Kuu Mhe Ignass Kitusi,daktari wa Rais Profesa Mohamed Janabi na Mtendaji Mkuu wa Mahakama
Chapisha Maoni