0
Serikali imekua ikipoteza mapato mengi
kutokana na utoroshwaji wa madini aina
ya Tanzanite yanayopatikana nchini
Tanzania pekee.
Kamishna wa Madini nchini,Eng Paul
Massanja amesema leo wakati wavmaonesho ya madini ya Vito yanayofanyika
jijini hapa ambayo yanahudhuriwa na
washiriki kutoka mataifa mbalimbali.
Amesema kwa takwimu za mwaka
2013,Tanzania ilipata dola za marekani 38 milioni wakati nchi ya Kenya ilijipatia kiasi cha dola 100 milioni na India ilijikusanyia kitita cha dola 300 milioni.

"Wote mnafahamu haya madini
yanapatikana Tanzania pekee huu ni
ushahidi kuwa kumekuwa na utoroshwaji
wa madini haya kwa kiwango kikubwa
jambo linalotunyima mapato ya
kutosha"anasema Eng Massanja
Hata hivyo amesema wataendelea kudhibiti mianya ya utoroshaji wa madini nje ya nchi
ambayo hayajaripiwa kodi sitahili huku
kukiwa na mipango ya kujenga jengo kubwa ambalo litatumika kufanyia biashara ya madini.Naibu Katibu Mkuu,Wizara ya Nishati na
Madini,Mhandisi Ngosi Mwihava
(katikati)akikata utepe kufungua Maonesho ya Tatu ya Madini ya Vito ya kimataifa mkoani Arusha leo.

Chapisha Maoni

 
Top