0
MABINGWA wa Afrika, Nigeria leo wametema rasmi taji baada ya kushindwa kufuzu kwenye Fainali zijazo za Mataifa ya Afrika kufuatia kulazimishwa sare ya 2-2 nyumbani na Afrika Kusini katika mchezo wa Kundi A.
Bafana Bafana imeifanyia 'roho mbaya' tu Nigeria kwani ilikuwa imekwishafuzu na katika mchezo wa leo, iliongoza muda mrefu kwa mabao 2-0 kabla ya wenyeji kusawazisha dakika za mwishoni.

Nigeria sasa haitakwenda Equatorial Guinea Januari mwakani kutetea taji lao, baada ya Kongo kuilaza 1-0 Sudan mjini Kharotum na kuungana na Bafana kwenda AFCON, huku Super Eagles ikimaliza katika nafasi ya tatu.

Chapisha Maoni

 
Top