0
NAHODHA wa AS Roma, Francesco Totti
amemuwashia moto mshambuliaji wa Liverpool, Mario Balotelli, akikuambia kwamba; 'hamsikilizi mtu yeyote.'
Totti alitolewa nje kwa kadi nyekundu kwa kumpiga mshambuliaji huyo alipokuwa anachezea Inter Milan miaka minne iliyopita wakati Roma ikifungwa 1-0 katika fainali ya Coppa Italia.

Na iantokea hajabadilisha maoni yake juu ya mchezaji huyo baada ya kunukuliwa akisema: "Siwezi kumshauri Balotelli. Kila mmoja amejaribu pia, lakini hamsikilizi mtu yeyote,".Maneno hayo yanakuja baada ya kocha wa Italia, Antonio Conte, aliyekaririwa na Raisport kabla ya mechi ya kirafiki na Albania akisema: "Siwezi kusema niko tofauti sana na makocha wengine wakubwa, lakini historia inatuambia kwamba walishindwa kumbadili
Balotelli. Itakuwa ni juu ya mchezaji mwenyewe, lakini sina muda sana na nahitaji vitu sahihi,".

Balotelli amekuwa katika wakati mgumu tangu ajiunge na Liverpool akitokea AC Milan mwezi Agosti kutokana na kufunga mabao mawili tu, moja katika Ligi ya Mabingwa na lingine katika
Kombe la Ligi.

Chapisha Maoni

 
Top