0
MSANII wa filamu za kibongo, Rachel Haule ‘Recho’ hivi karibuni aligeuka kituko baada ya kutupia picha ya nusu utupu katika mtandao wa kijamii.

Picha hiyo ambayo Recho amevaa shati tupu (inayoonesha ndani) bila kuvaa kitu kingine chochote, aliitupia kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram ambapo mashabiki na marafiki zake
walichangia huku wakimlaumu kuwa hakufanya vizuri kuiweka picha hiyo ya aibu mtandaoni.

Paparazi wetu alimuuliza Recho kulikoni? Akajibu hivi: “Nawapenda sana marafiki zangu lakini mimi sijaona tatizo la hii picha kwa sababu ni ya kawaida sana sioni ubaya wake.”


GPL

Chapisha Maoni

 
Top