NAHODHA wa Bayern Munich, Philipp Lahm atafanyiwa upasuaji baada ya kuvunjika kifundo chake cha mguu wa kulia leo na anatarajiwa kuwa nje kwa miezi mitatu.
Nahodha huyo wa Bayern, ambaye alistaafu soka ya kimataifa baada ya Kombe la Dunia Julai mwaka huu, aliumia katika mazoezi ya asubuhi na akalazimika kutolewa nje kwa
machela.
"Lahm amevunjika kifundo chake mguu wa kulia na atahitaji kwenda kufanyiwa upasuaji mapema," imesema Bayern katika taarifa yake.
"Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 atakuwa nje kwa miezi miwili na nusu hadi mitatu,".
Chapisha Maoni