Wimbi la utekaji na mauaji ya watoto katika Jiji la Dar bado ni tishio kufuatia wiki iliyopita, maiti ya mtoto Nuru Mohamed (7) mkazi wa Majohe
Kichangani Wilaya ya Ilala, kuokotwa ikiwa imeharibika vibaya, tena baadhi ya viungo vyake vikiwa vimenyofolewa.
Tukio hilo la kusikitisha lilitokea Novemba 6, mwaka huu, majira ya saa 12 jioni, baada ya watoto wenzake aliokuwa akicheza nao kudai kuwa Nuru alichukuliwa na mtu aliyekuwa
amevalia mavazi ya Kininja na kutokomea naye.
Baadhi ya mashuhuda waliokuwa eneo la tukio, walisema mwili wa mtoto huyo ulikutwa ukiwa hauna sehemu za siri, matiti, nyama ya kisogoni na makalio kukatwa na kuzibwa na gundi hali
iliyoashiria ushirikina.
“Nakumbuka siku ya kutoweka kwake, nilikua kazini nikapigiwa simu saa 12.45 jioni na kuelezwa Nuru ametekwa na mtu aliyevaa kininja, aliyemrubuni kwenda kumnunulia biskuti.
“Nilielezwa kwamba muda mfupi baada ya kutoweka, watoto wenzake walipatwa na hofu na kumwambia mama yake kwamba kuna mtu kaondoka na marehemu hali iliyomfanya kuinuka
na kuanza kufuatilia bila mafanikio.
“Niliungana na mke wangu pamoja na ndugu wengine kumtafuta hadi asubuhi bila mafanikio, nikiwa nipo maeneo ya Chamazi saa 2 asubuhi nilipigiwa simu na kuambiwa mwili wa mwanangu
umepatikana maeneo ya lwa Mkandawile ukiwa umeharibika, nilienda na kukuta kuwa ni yeye.
“Tulitoa taarifa polisi ambao walifika eneo la tukio na kuuchukua mwili hadi Hospitali ya Amana na muda mfupi baada ya kufanyiwa uchunguzi na
madaktari tuliuchukua na kuuzika makaburi yaliyopo maeneo ya ninakoishi,” alisema.
Mjunbe wa Shina namba 15 Tawi la Majohe, Matanzira Thomas maarufu kwa jina la Kobra alisema kwamba matukio hayo ya utekaji watoto, kuwaua na kuondoka na sehemu ya viungo ni
hatari hasa katika nchi ya amani kama Tanzania, hivyo ameliomba jeshi la polisi kufanya uchunguzi wa kina ili kuwabaini na kuwakamata watu hao
hatari.
Chapisha Maoni