0
WAZIRI MKUU

- Kamati imesema imejiridhisha pasipo mashaka kuwa, Waziri Mkuu, alikuwa ana taarifa zote kuhusiana na mchakato mzima wa kuchotwa fedha kutoka katika akaunti ya ESCROW.

-Kamati, kwa kuzingatia kielelezo namba 22, inathibitisha bila shaka kwamba, Waziri Mkuu alikuwa analijua jambo hili vizuri na kwamba aliridhia muamala huu ufanyike. Ndiyo maana katika maelezo yake ya Bungeni mara kadhaa
Waziri Mkuu alithibitisha kuwa fedha za Escrow hazikuwa fedha za Umma.

- Ripoti yasema ni jambo la kushangaza kuona kwamba, jambo kubwa na zito kama hili lingeweza kufanyika bila ya mamlaka za juu, hususan Mhe. Waziri Mkuu kufahamu.

-Yaongeza kuwa kwa uzito na unyeti wa jambo hili, vyovyote vile, Waziri Mkuu anapaswa kuwajibika kwa kauli zake na kwa kutokutekeleza wajibu wake wa kikatiba ipasavyo, ili kurejesha
imani ya wananchi kwa serikali yao na viongozi wao wa kisiasa.

MWANASHERIA MKUU

-Kamati imethibitisha kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali alitoa ushauri ulioipotosha Benki Kuu ya
Tanzania kuhusiana na hukumu ya Jaji Utamwa J.
Kwa kutumia madaraka yake vibaya, Mwanasheria Mkuu wa Serikali aliagiza kodi ya Serikali yenye thamani ya shilingi 21 bilioni isilipwe 107 na
hivyo kuikosesha Serikali mapato adhimu.

- Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kujua na kwa makusudi alilipotosha Bunge na Taifa kwamba mgogoro uliopelekea kufunguliwa kwa
Akaunti ya ESCROW ulikuwa ni mgogoro wa Wanahisa wa IPTL badala ya mgogoro kati ya TANESCO na IPTL.

-Kamati inapendekeza kuwa uteuzi wa
Mwanasheria Mkuu wa Serikali utenguliwe mara moja na kisha afikishwe mahakamani kwa matumizi mabaya ya Ofisi yaliyopelekea Serikali
kupoteza mabilioni ya fedha.
Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo.

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI

- Kamati imethibitisha kuwa Waziri wa Nishati na Madini amekuwa, mara kwa mara, akilipotosha Bunge tukufu na Taifa kwa ujumla kuhusiana na
Fedha za Akaunti ya Tegeta ESCROW kwamba ndani ya fedha hizo hakukuwa na fedha za umma. Hata mtu wa kawaida angeweza kujua kwamba
washirika wa ‘Tegeta Escrow Account’ ni akina nani na masharti ya kutoka kwa fedha hizo kwenye akaunti ni yapi kwa mujibu wa Mkataba wa uendeshaji wa akaunti hiyo.

-Hata hivyo, katika hali ya kushangaza, aidha kwa makusudi ama kwa sababu anazozijua vizuri zaidi mwenyewe, Waziri wa Nishati ananukuliwa kwenye
kumbukumbu rasmi za Bunge, Kwa nguvu kubwa na kwa kujiamini, akitetea uchotwaji wa fedha hizo kinyume na masharti ya Mkataba wa Escrow.

-Aidha, Kamati imebaini kuwa Waziri wa Nishati na Madini ndiye alikuwa dalali mkuu aliyewakutanisha Bwana Harbinder Singh Sethi na Bwana James Rugemalira, tena katika ofisi ya
Umma; na pengine hii ndiyo iliyokuwa sababu ya upotoshaji huu. Waziri wa Nishati na Madini alifanya udalali huo akijua dhahiri kuwa Bwana Sethi hana uhalali wa kisheria kufanya biashara
kwa jina la IPTL.

-Iwapo Waziri wa Nishati na Madini angetimiza wajibu wake ipasavyo, Fedha za Tegeta ESCROW zisingelipwa kwa watu wasiohusika, na Nchi ingeweza kuokoa mabilioni yaliyopotea kama kodi
za VAT, Capital Gain Tax na Ushuru wa Stempu ambazo ni sawa na takribani shilingi bilioni 30. -Kamati inapendekeza kuwa Mamlaka yake ya uteuzi itengue uteuzi wa Waziri wa Nishati na
Madini kutokana sababu hizo zilizoelezwa.

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI

-Kamati imethibitisha kuwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini alisema uongo Bungeni kwa kutamka kauli zilizokuwa na lengo la kupotosha umma kuhusu akaunti ya Tegeta ESCROW ikiwemo kutoa kauli ambazo zingeweza
kusababisha Nchi kuingia kwenye mgogoro wa kidiplomasia na nchi ya Uingereza.

-Kamati inapendekeza kuwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini achukuliwe hatua kali za kinidhamu ikiwemo kutenguliwa uteuzi wake. -Kamati pia inapendekeza kuwa Naibu Waziri
huyu afikishwe mbele ya Kamati ya Bunge ya Maadili ili aadhibiwe kama Mbunge kwa kusema uwongo Bungeni ili liwe fundisho kwa wabunge wengine kuhusiana na kauli wanazotoa ndani ya
Bunge lako tukufu.

KATIBU MKUU WA WIZARA YA NISHATI NA MADINI

-Kamati imethibitisha kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini aliingia makubaliano ya kutoa fedha katika Akaunti ya Tegeta ESCROW bila kujiridhisha kikamilifu kuwa maamuzi ya
hukumu ya ICSID 2 yalikuwa bado kutolewa na hivyo kusababisha fedha kutolewa bila kukokotoa upya gharama za ‘capacity charges’, jambo
ambalo limesababisha kupoteza fedha za umma.

-Vile vile, Kamati imebaini kuwa, Katibu Mkuu hakufanya uchunguzi wa kina (due diligence) kujiridhisha uhalali wa Kampuni ya Mechmar kuuzwa kwa Piperlink na baadaye kuuzwa kwa
PAP, na hivyo kusababisha fedha za akaunti ya Tegeta ESCROW kulipwa kwa asiyestahili na kinyume cha Mkataba wa akaunti ya Escrow.

-Kwa maana hiyo, Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini, pengine kwa uzembe wake ama kwa kukusudia kwa sababu anazozijua yeye mwenyewe zaidi, amesaidia uchotwaji na hatimaye utakatishaji wa fedha haramu.

-Kamati pia imethibitisha uzembe wa hali ya juu uliofanywa na Katibu Mkuu huyo, kushindwa kujiridhisha kama masharti ya Sheria ya kodi ya
Mapato Sura ya 333, Kifungu cha 90(2)
yalitekelezwa. Kifungu hicho kimsingi kinaitaka mamlaka ya ‘approval’’ ya uhamishaji wa Makampuni kutotambua Kampuni mpaka kwanza kodi za uhamishaji ziwe zimelipwa na hati za
malipo ya kodi zimetolewa na mamlaka ya kodi.

-Kamati inapendekeza kuwa uteuzi wa Katibu Mkuu huyu utenguliwe, na TAKUKURU wamfikishe mahakamani mara moja, kwa kuikosesha Serikali
Mapato, matumizi mabaya ya ofisi na kusaidia utakatishaji wa fedha haramu.

Chapisha Maoni

 
Top