Serikali ya Tanzania imesema ipo kwenye mchakato wa kuandaa adhabu mbadala kwa wahalifu wa makosa madogo madogo ili kupunguza msongamano magerezani ambao kwa
sasa unapelekea hali mbaya katika Magereza hayo.
Akijibu swali bungeni mjini Dodoma jana kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Utumishi Bi. Celina Kombani amesema hali ya msongamano kwa sasa katika magereza inatokana na Majengo yake
kuwa ni ya muda mrefu na yalikuwa
yanatosheleza katika kipindi yalipojengwa.
Kombani amesema kuwa kwa sasa Serikali ipo katika mchakato wa kuboresha Magereza hayo kwa bajeti iliyopo ila kwa sasa kitakachofanyika ni
kutoa adhababu mbadala kwa wafungwa wenye makosa madogo madogo ikiwemo vifungo vya
nje.
Chapisha Maoni