Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein amesema hajatangaza kugombea au kutogombea Uraisi kwa Awamu nyingine visiwani humo na wanaomtangazia kuwa hagombei tena waache kudanganya.
Dkt. Shein ametoa kauli hiyo Visiwani humo wakati akizungumza na viongozi na wanachama wa CCM, ikiwa ni miongoni mwa mikakakati ya kuimarisha chama ambapo amesema kuna watu wameanza kutangaza kuwa yeye hatagombea tena
Urais.
Aidha Dkt. Shein amewataka wanachama hao kuwa makini na kukijenga chama huku akisisitiza
umuhimu wa mashina na maskani za chama kwa vile zinatambuliwa ndani ya katiba ya chama hicho.
Aidha Dkt. Shein amesema kuwa wanachama wa CCM, Mkoani humo hawana budi kuhawasisha juu ya upigaji wa kura ya ndio katika katiba inayopendekezwa kwa kuwa imejaa maslahi kwa Wanzanzibar.
Chapisha Maoni