Wamiliki wa Blogs nchini wametakiwa kuzitumia vyema blog zao katika kuripoti habari na matukio mbalimbali wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa, wabunge na urais.
Hayo yamesemwa na Mkurugezi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Profesa John Nkoma jana alipokuwa akizungumza na wamiliki wa Blogs katika Ukumbi wa Mlimani City
jijini Dar es Salaam.
Profesa Nkoma alisisitiza kwamba wakati wa uchaguzi wamiliki wa Blogs wanatakiwa kutoa fursa sawa kwa kila upande pasipo upendeleo wowote wala uchochezi.
Aidha katika mkutao huo, wamiliki wa Blogs walikubaliana kuendeleza mchakato wa kuwa na umoja wao uliosajiliwa kisheria ambapo
walichagua viongozi wa muda watakaosimamia mchakato huo.
Mwandishi wa gazeti la Jamboleo kutoka mkoani Iringa Bw Francis Godwin aliteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa chama cha Wamiliki wa Mitandao
ya Kijamii (Blogs) nchini Tanzania.
Godwin ambae ni mmiliki wa blog ya
"MatukioDaima" na "FrancisGodwin" aliteuliwa katika nafasi hiyo kama mwakilishi wa wamiliki wote wa blogs za mikoani, huku Joachim Mushi
akiteuliwa kuwa mwenyekiti wa chama hicho.
Wengine walioteuliwa ni pamoja na Katibu wa chama hicho Khadija Kalili, ambapo wajumbe ni Mdimu Henry, William Malecela, Othman Maulid
na Shamim Mwasha.
Akizungumza mara baada ya uteuzi huo
mwenyekiti wa chama hicho Bw Mushi alisema kuwa lengo ni kuhakikisha katiba ya chama hicho inakamilika mapema zaidi ili chama hicho kiweze
kusajiliwa rasmi.
Safu ya Uongozi:
1.Joachim Mushi - Mwenyekiti
2. Francis Godwin - Makamu Mwenyekiti
3. Khadija Kalili - Katibu
4. Shamim Mwasha - Mjumbe
5. Othman Maulid - Mjumbe
6. William Malecela 'Lemutuz'- Mjumbe
7.Henry Mdimu - Mjumbe
Chapisha Maoni