0
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda amesema Serikali itafanya mabadiliko ya kiutawala katika ngazi mbalimbali Wilaya ya Kiteto na Mkoa wa Manyara wiki hii ili kuimarisha uongozi kukabiliana na
mauaji ya wakulima na wafugaji yaliyosababisha vifo vya watu 17 tangu Januari 12 mwaka huu
hadi sasa.

Pinda alisema hayo bungeni mjini Dodoma jana wakati akitoa taarifa kuhusu vurugu zinazoendelea Kiteto kati ya wafugaji na wakulima na kusababisha mauaji.

Alisema mabadiliko ya uongozi wa kiutawala katika eneo hilo ni moja ya hatua ambazo zinachukuliwa kitaifa nyingine zikiwa ni kuendelea kutoa elimu kwa umma juu ya kuondoa na
kuepuka na kutatua migogoro inayojitokeza kwa njia ya amani.

“Kupanga mipango ya maeneo mbalimbali wilayani Kiteto na kutatua migogoro inayojitokeza kwa kushirikisha viongozi wa makundi mbalimbali
ya kijamii kama vile malaigwanani, wazee wa kimila na viongozi wa dini,” alisema Pinda.

Alisema jambo lingine ni kupanga matumizi bora ya ardhi na upimaji wake katika matumizi mbalimbali na kuimilikisha kwa wananchi. Pinda alisema hali ya mauaji Kiteto imekuwa ni ya kujirudia, kwani Januari 12 mwaka huu, wafugaji walifanya mashambulizi ya silaha za moto na za jadi kwa wafugaji na kusababisha vifo vya watu
10, kuteketeza pikipiki sita na mabanda 53 kuchomwa kitu ambacho kilionyesha kuwa mauaji hayo yalikuwa ya kupanga.

Pinda alisema Novemba 11, mwaka huu katika Kijiji cha Matui, mapigano ya wakulima na wafugaji yalitokea na kusababisha vifo vya watu watano na Novemba 13 katika Kijiji cha Chekanao,
wakulima wawili waliuawa na maboma 13 kuchomwa.

“Pamoja na hali hiyo kudhibtiwa katika vijiji hivyo, bado wananchi wana hofu juu ya maisha yao,” alisema Pinda.
Alisema Polisi Makao Makuu Dar es Salaam imetuma askari wake Mkoa wa Manyara.

Chapisha Maoni

 
Top