Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akitoa hotuba ya ufunguzi wa Mkutano wa Kimataifa wa siku mbili kuhusu Sauti ya Kwanza ya Sayansi ya Jamii. Mkutano huo ambao unafanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani chini ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam unawashirikisha Wajumbe kutoka Tanzania, Kenya, Uganda, Ghana, Nigeria na Canada. Katika hotuba yake Mhe.
Membe alisisitiza umuhimu wa Wasomi na Wanazuoni kujikita katika Tafiti za Kisayansi ili kuja na majibu yatakayoisaidia nchi kuondokana na umaskini, utunzaji wa mazingira na masuala mengine ya manufaa kwa nchi.
Chapisha Maoni