0
KOCHA wa Arsenal, Mfaransa Arsener Wenger amesema klabu hiyo haina mpango wa kumuuza mshambuliajinwake, Lukas Padolski.
Wenger amesistiza kwamba Podolski hatauzwa, licha ya taarifa kwamba mshambuliaji huyo wa Ujerumani anataka kuondoka katika klabu hiyo.

Bosi huyo wa amezipuuza habari zinazoandikwa mfululizo kwamba Podolski ataondoka Arsenal
kwa dau la Euro Milioni 5 ifikapo Januari, kwa kusema; "Ni za kutengenezwa kabisa,".Lukas Podolski aliichezea nchi yake dhidi ya Gibraltar wiki hii, lakini amekuwa akisotea namba Arsenal



"Yeye (Podolski) hauzwi," Wenger amesema na kuongeza. "Mimi ndiye mtu ninayepanga bei, amerudi kutoka Kombe la Dunia, anacheza nafasi ambayo nina wachezaji wengine, anatakiwa kushindani namba,"amesema.

Chapisha Maoni

 
Top