0
Timu ya Yanga leo imefungwa 1-0 na
Kagera Sugar katika Uwanja wa Kaitaba
katika Ligi Kuu ya Vodacom, mjini Bukoba, Kagera.

Klabu ya Dar es salaam Young Afrika
imekubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa wenyeji wao Kagera Sugar kwenye mchezo uliopigwa ndani ya Uwanja wa Kaitaba Mjini Bukoba.

Kipindi cha kwanza Timu zote mbili
zilimaliza bila ya kufungana, Kipindi cha
pili Kagera Sugar walitumia faida ya
kucheza nyumbani na kufanikiwa kupata
bao lililofungwa kiufundi na paul Ngwai
na kuibuka na ushindi huo wa bao 1-0 na kuwaacha Yanga wakibaki na pointi zao 10 ambazo wamevuna katika michezo 6.

Chapisha Maoni

 
Top