0
CHELSEA imejiimarisha kileleni mwa Ligi Kuu ya England kufuatia ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Queens Park Rangers jioni ya leo Uwanja wa Smtamfrod Bridge, London.

Ushindi huo, unaifanya timu ya Jose
Mourinho itimize pointi 26 baada ya kucheza mechi 10,ikiizidi kwa pointi nne Southampton katika nafasi ya pili na pointi tisa mabingwa watetezi, Manchester City walio nafasi ya
tatu.

Oscar dos Santos Emboaba Junior aliifungia bao la kwanza The Blues dakika ya 32 kabla ya Charlie Austin kuisawazishia QPR dakika
ya 62- na Eden Hazard kufunga la ushindi kwa penalti dakika ya 75.

Kikosi cha Chelsea kilikuwa; Courtois,
Ivanovic, Cahill, Terry, Filipe Luis, Matic,
Fabregas, Willian/Drogba dk64, Oscar,
Hazard/Ramires dk90 na Diego Costa/
Schurrle dk78.

QPR; Green, Isla, Caulker, Dunne, Suk-Young, Vargas, Henry, Sandro, Fer/Traore dk83, Hoilett/Zamora dk60 na Austin.

Chapisha Maoni

 
Top