WAKURUGENZI wa bendi hasimu za dansi Tanzania, African Stars, Asha Baraka na Extra Bongo, Ali Choki, leo wameongoza mamia ya waombolezaji kumzika aliyekuwa mnenguaji wa zamani wa bendi hizo, Aisha
Mohamed Mbegu ‘Aisha Madinda’.
Mohamed Mbegu ‘Aisha Madinda’.
Mazishi ya Aisha Madinda yamefanyika leo kwenye Makaburi ya Kijiji cha Mikwambe, Kigamboni jijini Dar es Salaam, baada ya kukwama kufanyika jana kutokana na zuio la Jeshi la Polisi, kupisha uchunguzi wa sababu za kifo cha ghafla cha mnenguaji huyo.
Baada ya uchunguzi huo kufanyika na
ripoti kukabidhiwa kwa Jeshi la Polisi na
familia, mazishi hayo yakafanyika leo jioni yakihudhuriwa na Asha Baraka na Choki, pamoja na Makamu wa Rais wa Shirikisho la Muziki Tanzania, Salim Omari Mwinyi.
Akizungumza katika mazishi hayo, Asha
Baraka ambaye ni Mkurugenzi wa African Stars Entertainment inayoimiliki Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’, alimuelezea Aisha kuwa ni sawa na mwanaye kutokana na muda mwingi aliotumia akiwa Twanga.
Baraka aliongeza kuwa licha ya kutokuwa na Aisha katika siku za karibuni, bado Twanga Pepeta inatambua na kuthamini
mchango wa mkali huyo wa jukwaa na
kwamba pengo lake halitasahaulika
kirahisi ndani ya bendi hiyo kongwe.
Kwa upande wake Choki alisema daima
atakumbuka uwajibikaji, usikivu na upendo wa Aisha akiwa na Extra Bongo ‘Wazee wa Kizigo,’ na kwamba kwake yeye marehemu ni sawa na dada yake, huku akimtaja kama mtumishi mwema.
“Alikuwa na Extra Bongo kwa muda mfupi, lakini aina yake ya utumishi utabaki katika kumbukumbu zetu daima.
Huu ni mwaka wa taabu kwangu, kwani siku ya arobaini ya marehemu mke wangu, alifariki pia mzee
wangu Shem Karenga,” alisikitika Choki.
Choki alienda mbali zaidi kwa kulalama
kuwa, siku moja baada ya kumzika Shem Karenga, ndio siku aliyofariki Aisha Madinda, hivyo kuendeleza mfululizo wa majonzi kwake na wadau wa tasnia nzima ya muziki wa dansi nchini.
wangu Shem Karenga,” alisikitika Choki.
Choki alienda mbali zaidi kwa kulalama
kuwa, siku moja baada ya kumzika Shem Karenga, ndio siku aliyofariki Aisha Madinda, hivyo kuendeleza mfululizo wa majonzi kwake na wadau wa tasnia nzima ya muziki wa dansi nchini.
Kwa upande wake, mtoto wa dada wa
marehemu, Sheikh Mohamed Mussa, ambaye aliongoza mazishi upande wa familia, aliwashukuru Watanzania kwa ushirikiano walioutoa katika kufanikisha mazishi hayo, huku akiwataka kuuendelea kumuombea.
Mwili wa Aisha Madinda ukitolewa kwenye gari la kubebea maiti mara baada ya kuwasili nyumbani kwao,Kigamboni.
Mwili wa Aisha Madinda ukiwasili
nyumbani kwa ajili ya kuswaliwa kabla ya mazishi yaliyofanyika katika makaburi ya Kibada, Kigamboni jijini Dar es salaam jioni hii.
Chapisha Maoni