Klabu ya Yanga imemtaja, Dr Jonas
Tiboroha (45) kuwa katibu mkuu wa klabu na kuwathibitisha rasmi Hans van Der Pluijm na Charles Mkwassa kuwa makocha wapya sambamba na kuitaka sekretarieti iliyomaliza muda wake kukabidhi ofisi haraka.
Pluijm na Mkwassa wanachukua nafasi ya makocha wa Yanga, Marcio Maximo na Leonardo Neiva waliotupiwa virago huku Tiboraha akichukua mikoba ya Beno Njovu aliyemaliza muda wake.
Awali mkufunzi wa Fifa, Henry Tandau
alipigiwa chapuo kuchukua cheo cha
Ukatibu baada ya Njovu licha ya kushindwa kufikia muafaka na viongozi na Tandau kukataa kuajiliwa na Yanga.
Akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo , Jerry Muro alisema Tiboraha ataiongoza sekretarietri mpya ya klabu hiyo.
"Uteuzi wa sekretarieti hiyo
umependekezwa kwa kuzingatia vigezo na itaongozwa na Tiboraha ambaye atafanya kazi na mkuu wa Idara ya habari ambaye ni mimi, Omar Kaya yeye anakuwa Mkuu wa Idara ya Masoko,Frank Chacha anakuwa mkuu wa Idara ya Sheria na Baraka Deusdedit anakuwa Mkuu wa Idara ya Fedha," alisema Murro.
Akizungumzia suala la makocha Pluijm na Mkwassa, Murro alisema makocha hao wataanza kazi mara moja na kusisitiza kuwa tayari klabu hiyo imeachana na Maximo na Neiva.
"Maximo na Neiva sio makocha tena wa
Yanga," alisema Murro ambaye hakuwa
tayari kuweka wazi kama klabu hiyo
imemalizana na makocha hao baada ya
kuvunja nao mkataba zaidi ya kueleza
benchi la ufundi litaongozwa na Pluijm
akisaidiana na Mkwassa.
"Mwenyekiti wa Yanga pia anapenda
kuchukua fursa hii kuwashukuru Maximo pamoja na Neiva kwa ushirikiano wao katika kufundisha timu ya Yanga kwa muda wa miezi sita iliyopita, na anawatakia kila kheri katika safari yao na Mungu akipenda wataendelea kushirikiana nasi katika siku za mbeleni.
"Pamoja na hayo, Mwenyekiti anapenda
kuwashukuru wafanyakazi wa Sekretariati iliyomaliza muda wake, japo bado wapo kwenye mchakato wa kukabidhi ofisi zao, na angependa kuwasihi wamalize haraka
makabidhiano yao," alisema Murro katika taarifa hiyo na kuongeza.
"Niwafahamishe wana Yanga kuwa uongozi umeamua kuongeza vijana zaidi kwenye uongozi, ili muda wa kustaafu madarakani ukifika Klabu ya Yanga itakuwa na warithi bora watakaoendeleza mazuri waliokuta.

Chapisha Maoni