0
Waziri wa Fedha Mh. Saada Mkuya Salum (katikati) akizindua rasmi Takwimu za Pato la Taifa zilizorekebishwa kwa mwaka
wa kizio wa 2007 leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Fedha Mh. Saada Mkuya Salum (kulia) akimkabidhi Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servicius Likwelile chapisho la lenye Takwimu za Pato la Taifa zilizorekebishwa kwa mwaka wa kizio wa 2007 wakati wa uzinduzi wa usambazaji wa takwimu hizo leo jijini Dar es salaam.
 Baadhi ya viongozi na wageni
waliohudhuria uzinduzi wa usambazaji wa Takwimu za Pato la Taifa zilizorekebishwa kwa mwaka wa kizio wa 2007 wakimsikiliza Meneja wa Takwimu za Pato la Taifa, Bw. Daniel Masolwa wakati akiwasilisha mada kuhusu Pato la Taifa leo jijini Dar es salaam.



.................................................................

Serikali imesema kuwa Pato la Taifa kwa
mwaka 2007 limeongezeka hadi kufikia
shilingi trilioni 26.8 ikilinganishwa na
trilioni 20.9 za mwaka 2001, ambapo
wastani wa pato la mwananchi mmoja
mmoja limeongezeka kutoka shilingi
milioni1,186,200/= mwaka 2001 hadi shilingi milioni 1, 561,050/= mwaka 2013.

Akizindua usambazaji wa takwimu hizo leo jijini Dar es salaam, Waziri wa Fedha Mh. Saada Mkuya Salum ameeleza kuwa
matokeo hayo ni sawa na ongezeko la
ukubwa wa Pato la Taifa kwa asilimia
27.8. Amesema ongezeko hilo ni matokeo ya juhudi za Serikali kuweka mazingira mazuri na kutengeneza fursa za kuwawezesha wananchi kufanya kazi za kujiajiri na hatimaye kupata kipato halali kwa kazi wanazofanya.

Mh. Mkuya amesema kuwa kukua kwa
uchumi wa Tanzania kumechangiwa na
kujumuishwa kwa shughuli mbalimbali
zikiwemo Sayansi na Teknolojia ambako
kumetoa fursa kwa wananchi kujiongezea kipato hususan matumizi ya simu za kiganjani ambazo zimerahisisha
mawasiliano na utafutaji wa masoko ya
bidhaa ndani na nje ya nchi.

Amezitaja shughuli nyingine kuwa ni
ukamilishaji wa miamala mbalimbali ya
kibenki na mikopo ambazo zimekuzwa na sekta ya mawasiliano , kuongeza ajira na kupunguza muda wa kusubiri huduma za malipo katika maeneo mbalimbali nchini.

Aidha, amefafanua kuwa kuongezeka kwa thamani ya Pato la Taifa kunaiongezea Serikali uwezo kimapato kupitia kodi na kuiwezesha kugharamia ujenzi wa miundombinu na utoaji wa huduma mbalimbali kwa wananchi.

“Serikali imeendelea kuimarisha
upatikanaji wa huduma ya maji safi na
salama, utafiti wa mapato na matumizi ya Kaya Binafsi ya mwaka 2012 unaonyesha asilimia 60 ya kaya zote nchini zinapata maji safi na salama hasa hususan maeneo ya mijini,zaidi ya asilimia 20 ya kaya zote nchini zinatumia nishati umeme haya ni mafanikio makubwa ya matokeo ya ukuaji wa uchumi nchini” Amesisitiza Mh. Mkuya.

Akizungumzia mchango wa Sekta Binafsi katika kukua kwa pato la taifa nchini amesema kuwa ajira zipatazo laki nne kati ya laki sita katika sekta iliyo rasmi zimepatikana.Kwa upande wake
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya
Takwimu Dkt. Albina Chuwa akizungumza wakati wa uzinduzi huo amesema kuwa kazi ya kurekebisha takwimu za Pato la Taifa imetumia Tafiti za Taifa zilizofanyika
kwa kipindi cha mwaka 2001 hadi 2007.
Amezitaja tafiti hizo kuwa ni pamoja na
utafiti wa mapato na matumizi ya Kaya wa mwaka 2007, Sensa ya Kilimo iliyofanyika mwaka 2008 na Takwimu nyingine za utawala kutoka katika Wizara na Idara za Serikali.

Aidha, amefafanua kuwa ukokotoaji wa
takwimu hizo umefuata mfumo wa Umoja wa Mataifa wa kutayarisha takwimu za Pato la Taifa wa mwaka 1993 na 2008 kwa lengo la kuhakikisha kuwa takwimu hizo zinalinganishwa na takwimu nyingine duniani.

Chapisha Maoni

 
Top