0
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA) kimepata pigo baada ya mapingamizi yake 155 kwa wagombea katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Jiji la Arusha kutupwa.

Mapingamizi hayo yaliwasilishwa kwa Katibu Tawala wilaya ya Arusha na msimamizi mkuu wa uchaguzi, Juma Iddy ambaye pia ni Mkurugenzi wa Jiji la Arusha kwa ajili ya kusikiliza rufaa.

Akitoa uamuzi huo juzi, Katibu Tawala wa Wilaya ya Arusha, Daniel Machunda alisema mapingamizi yaliyowasilishwa na Chadema, yalidai kuwa wagombea wa CCM walikuwa hawajadhaminiwa na
chama chao.

Machunda alisema mbali na hilo, mwisho wa kurudisha fomu ilikuwa Novemba 23 mwaka huu na mapingamizi yote yalitakiwa kuwasilishwa ndani ya siku mbili kuanzia Novemba 24, lakini
Chadema waliyawasilisha Novemba 26, hivyo kuwa nje ya muda uliopo kikanuni.

“Kwa mujibu wa kanuni ya uchaguzi wa
mwenyekiti wa mtaa na wajumbe wa kamati ya mtaa katika mamlaka za mji za mwaka 2014 (15) (2) kinasema;
“Pingamizi chini ya kanuni ndogo (1) ya kanuni hii itawasilishwa kwa maandishi kwa msimamizi msaidizi wa uchaguzi ndani ya siku mbili tangu kufanyika kwa uteuzi na msimamizi atatoa uamuzi
kwa muda usizidi siku mbili kwa kuanzia siku aliyopokea pingamizi hilo’’ alisema.

Alisema kwa mujibu wa kanuni hiyo mapingamizi yote ya Chadema yaliyowasilishwa Novemba 26 mwaka huu yalipelekwa nje ya muda na kwa
mantiki hiyo pingamizi hizo yametupiliwa mbali.

Akizungumzia hali hiyo, Katibu wa CCM wilaya ya Arusha, Feruz Juma alisema amefurahishwa na uamuzi huo. Mapingamizi hayo yaliwalenga wanaCCM wanaowania uongozi katika Kata za Kaloleni, Unga Ltd, Ngarenaro, Olerien na Levolosi.

Chapisha Maoni

 
Top