0
CHELSEA imeichapa mabao 2-0 Hull City katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Stamford Bridge, London jioni ya leo.

Eden Hazard alifunga bao la kwanza dakika ya saba kwa kichwa akiunganisha krosi ya Oscar, kabla ya Tom Huddlestone wa Hull kutolewa
kwa kadi nyekundu dakika ya 60 kwa
kumchezea rafu Filipe Luis.

Diego Costa akaifungia The Blues bao la pili dakika ya 68, ambalo linakuwa la kwanza ndani ya mechi nne na la 12 msimu huu.

Ushindi huo, unaifanya timu hiyo ya kocha Mreno, Jose Mourinho ipae kileleni kwa pointi tatu zaidi, dhidi ya mabingwa watetezi, Manchester City.

Kikosi cha Chelsea kilikuwa; Cech, Ivanovic, Cahill, Terry, Luis, Mikel, Matic, Willian, Oscar, Hazard na Costa.

Chapisha Maoni

 
Top