BAO pekee la kiungo mkongwe, Frank Lampard limeipa Manchester City ushindi wa 1-0 dhidi ya Leicester City
Uwanja wa King Power katika
mchezo wa Ligi Kuu ya England jioni ya leo. Kiungo huyo wa zamani wa Chelsea, alifunga dakika ya 40 ambalo linakuwa bao lake la 175 katika historia yake ya kucheza Ligi Kuu ya England na kumfikia nyota wa zamani wa Arsenal, Thierry Henry.
Katika mchezo wa leo, City iliyomkosa
mshambuliaji wake tegemeo, Sergio Aguero ambaye ni majeruhi, ilipata pigo lingine baada ya beki Vincent Kompany kuumia dakika ya 74.
Kikosi cha Leicester kilikuwa; Hamer, Simpson, Wasilewski, Morgan, Konchesky, Mahrez, King, Cambiasso, Drinkwater/Knockaert dk79,
Schlupp/Ulloa dk64 na Vardy/Powell dk73.
Manchester City; Hart, Sagna, Kompany/
Demichelis dk77, Mangala, Clichy, Fernando, Lampard/Milner dk60, Nasri, Toure, Silva na Pozo/Navas dk74.
Chapisha Maoni